Connect with us

Makala

Straika Simba Sc Atua Zesco United

Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Simba Sc Fredy Michael Koublan amesajili na klabu ya Zesco United inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Zambia kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mshambuliaji huyo ambaye aliichezea Simba sc kwa miezi sita pekee alisajili kutokea klabu ya Green Eagle Fc ya nchini Zambia ambapo baada ya kushindwa kuonyesha kiwango alivunjiwa mkataba na nafasi yake kuzibwa na Lionel Ateba.

Awali mshambuliaji huyo ilikua ajiunge na Mc Algers ya nchini Algeria lakini kigezo cha kutokua na nafasi katika timu ya Taifa ya Ivory coast kuliharibu dili hilo na hatimaye alirejea nchini na kisha kufanya mazoezi binafsi akiungana na mastaa mbalimbali wa kigeni nchini.

Klabu hiyo imethibitisha taarifa za kumsajili staa huyo kupitia mitandao yake ya kijamii ambapo ataanza rasmi kutumika baada ya dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala