Connect with us

Makala

Yanga Sc Wakimbia Chamazi Complex

Uongozi wa Klabu ya Yanga sc umetangaza kuuhama uwanja wa Azam Complex Chamazi katika michezo yote iliyosalia ya ligi kuu ya Nbc nchini kutokana na matokeo mabaya iliyoyapata hivi karibuni katika uwanja huo na sasa itautumia uwanja wa Kmc Complex.

Yanga sc imejikuta ikishuka mpaka nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu nchini baada ya kukubali vipigo viwili dhidi ya Azam Fc ambapo walifungwa 1-0 na dhidi ya Tabora United walipofungwa 3-1.

Katika kupambana na hali hiyo mabosi wa klabu hiyo walichukua uamuzi wa kuhamishia michezo yote iliyosalia ya ligi kuu katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Tayari klabu hiyo imeandika barua kwenda bodi ya ligi kuu nchini ambayo ndio wasimamizi wakuu wa ligi kuu ambapo bodi imethibitisha kupokea barua hiyo.

” Nathibitisha ni kweli Yanga wameleta barua ya kuomba kuhamia Uwanja wa KMC Complex kutokea Azam Complex na sisi kama Bodi barua hiyo tumeipokea jana na kwa sababu ilikua weekend hatukuweza kuifanyia kazi” Alisema mtendaji mkuu huyo wa kwanza tangu ianzishwe bodi hiyo.

“Leo ni Jumatatu tunatarajia kuendelea na kazi na kitu tutakachoanza nacho ni kuitolea maamuzi barua hiyo kutoka kwa Yanga”aliendelea kusema

“Hata mimi nimeona Yanga wametoa Taarifa kwa Umma kuhama uwanja, Siwezi kuwapangia nini cha kufanya kwa sababu hizi ni Taasisi mbili tofauti zinaendeshwa tofauti”

“Sisi leo tutakaa na tutatazama kanuni zinasemaje kisha tutatoa majibu kuhusu kile ambacho wao wamekiomba”Alimalizia kuelezea kuhusu suala hilo.

Hata hivyo ili suala la kuhama hama viwanja kwa klabu za Simba sc na Yanga sc limekua likitokea mara kwa mara ambapo linasababishwa na kukosa viwanja vyake ambapo mara nyingi wamekua wakitumia uwanja wa uhuru ama Benjamin Mkapa ambavyo sasa hivi viko kwenye matengenezo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala