Connect with us

Makala

Simba sc Yakomaa Kileleni mwa Ligi Kuu

Klabu ya Simba Sc imechukua alama tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Dodoma Jiji uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Simba sc ilianza mchezo na washambuliaji watatu ambapo Steven Mukwala,Lionel Ateba na Kibu Dennis huku Dodoma Jiji ikiwaanzisha Waziri Junior na Ibrahim Ajibu waliosaidiwa na Idd Kipangwile kutengeneza utatu hatari wa kushambulia wakilindwa na kiungo wa shoka Salmin Hoza na Appolo Otieno.

Simba sc mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza ilishindwa kupata bao lolote na kipindi cha pili timu zote zilirejea na nguvu mpya ambapo mashambulizi ya kasi yaliongezeka kila upande.

Mohammed Hussein alifanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kuamuru iwe penati ambayo ilifungwa na Jean Charles Ahoua dakika ya 63 ya mchezo huo mkali na lilidumu mpaka dakika ya mwisho ya mchezo huo.

Simba sc sasa imefikisha alama 12 ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini huku ikicheza michezo minne na Dodoma Jiji licha ya kucheza michezo sita imebaki nafasi ya kumi ya msimamo ikiwa na alama sita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala