Connect with us

Makala

Yanga sc Yakomaa na Kagoma

Klabu ya Yanga sc imeendelea kukomaa na usajili wa mchezaji Yusuph Kagoma ambaye amejiunga na Simba sc msimu huu ikisisitiza kuwa ni mchezaji wa klabu hiyo baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu klabuni hapo.

Kagoma aliyeuzwa na Fountain Gate Fc kwa Simba sc awali alifanya mazungumzo na Yanga sc na kusaini mkataba huo wa miaka mitatu baada ya klabu za Yanga sc n Fountain Gate kukubaliana kuhusu uhamisho wa kiungo huyo kwa dau la shilingi milioni 30 ambazo zilipaswa kulipwa kwa awamu mbili.

Kagoma baadae alibadili uamuzi na kusaini Simba sc huku Klabu ya Fountain Gate Fc ikiitarifu Yanga sc kuwa mchezaji huyo imemuuza Simba sc na tayari imetoa bashrua ya kumuachia rasmi.

Simon Patrick ambaye ni mwanasheria wa klabu ya Yanga sc amesema kuwa mchezaji huyo anapaswa kufungiwa kutokana na kusaini klabu mbili huku akisisitiza hatua muhimu matatu kuchukuliwa na Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ambao ndio wanasimamia kesi hiyo.

“Tunaiomba kamati itamke kuwa Yusuph Kagoma ni mchezaji wa Yanga sc na tumemnunua na tuna ushahidi kuwa tumemnunua kabla ya timu 30/4 na tumemnunua kutoka Fountain Gate Fc na ushahidi tunao”.Alisema Simon

Pia Simon aliendelea kusema kuwa”Tunaiomba Kamati kama ilivyokua ikisimamia sheria zingine isimamie pia na kanuni ya 42 ya kuhusu mchezaji aliyesaini timu mbili ipo pale”.

Na suala la tatu ambalo wakili huyo alisisitiza kwa kamati ni kuhusu fidia kwa klabu hiyo.

“Tunaiomba kamati itamke kuwa kitendo cha mchezaji huyu kusaini timu mbili ina maana kuwa mchezaji huyo amevunja mkataba wetu hivyo wanatakiwa watoe adhabu na fidia kwa mujibu wa mkataba”.Alimalizia kusema Simon Patrick

Kwa upande wa klabu za Simba sc na Fountain Gate Fc zenyewe zimeendelea kusisitiza kuwa mchezaji huyo ni mali ya Simba Sc na zilifuata taratibu rasmi za usajili.

Mpaka sasa mchezaji huyo ameenda nchini Libya na kikosi cha klabu ya Simba Sc kwa ajili ya kucheza michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala