Connect with us

Makala

Azam Fc Vs Pamba Jiji Kupigwa Septemba 14

Mchezo wa ligi kuu ya soka ya Nbc nchini baina ya Azam Fc dhidi ya Pamba Jiji sasa utachezwa siku ya Jumamosi Septemba 14 badala ya Ijumaa Septemba 13 katika uwanja wa Chamazi Complex uliopo jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi kuu nchini inasema kuwa mchezo huo umesogezwa mbele kutokana na matakwa ya mdhamini wa ligi Azam Tv ili aweze kujipanga kurusha matangazo hayo kwa ufanisi zaidi.

Pia kutokana na baadhi ya wachezaji wa klabu ya Azam Fc kama Feisal Salum,Lusajo Mwaikenda na Paschal Msindo ambao nao wanatarajiwa kurejea kuungana na kikosi hicho hii leo wakitoka timu ya Taifa ya Tanzania iliyokua nchini Ivory coast ikicheza na Guinea kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika 2025 nchini Morocco.

Katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Tanzania Pamba Jiji ipo nafasi ya saba ikiwa na alama mbili huku ikiwa imecheza michezo miwili na Azam Fc ikiwa nafasi ya kumi na moja ikiwa na alama moja ikicheza mchezo mmoja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala