Connect with us

Makala

Fadlu,Ahoua Walamba Tuzo za August

Kocha wa Klabu ya Simba Sc Fadlu Davis sambamba na kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Jean Charles Ahoua wameibuka kuwa Kocha bora na mchezaji bora wa ligi kuu ya Nbc nchini kwa mwezi huu wa nane.

Waajiriwa hao wa klabu ya Simba Sc wamelamba tuzo hizo mapema hivi leo ambapo wametangazwa na bodi ya ligi kuu nchini ambayo hufanya tathmini kuhusu nani anafaa kuchukua tuzo hizo.

Tplb katika taarifa yake kwa umma imetangaza kuwa Fadlu amepata nafasi hiyo baada ya kuwezesha Simba sc kuchukua alama sita na mabao saba ambapo ilifanikiwa kushinda michezo miwili mfululizo ya ligi kuu dhidi ya Tabora United na Fountain Gate Fc.

Ahoua yeye alifanikiwa kufunga bao moja huku akitoa usaidizi wa upatikanaji wa mabao matatu katika michezo hiyo miwili ya ligi kuu ya Nbc.

Mpaka sasa ambapo ligi Imesimama Simba sc imejikita kileleni mwa msimamo ikiwa na alama sita na mabao saba katika michezo miwili ya ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala