Connect with us

Makala

Azam Fc Yatangaza Rasmi Kuachana na Dabo

Klabu ya Azam Fc hatimaye imetangaza rasmi kuachana na kocha wake mkuu Yousouph Dabo kwa makubaliano ya pande mbili kutokana na mwenendo usioridhisha wa kikosi hicho.

Awali tetesi zilisambaa kuwa mabosi wa klabu hiyo wapo mbioni kuachana na kocha huyo baada ya kufungwa 4-1 na Yanga sc katika fainali ya kombe la ngao ya jamii kisha kutolewa katika michuano ya kombe la Klabu bingwa barani Afrika na Apr baada ya kukubali kipigo cha 2-0 ugenini katika mchezo wa marudiano.

Kama hiyo haitoshi bado Dabo alishindwa kupata ushindi katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Nbc kwa timu hiyo ambapo ilipata Suluhu ugenini dhidi ya Jkt Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na vyanzo rasmi vya klabu hiyo inasema kuwa kikosi cha timu hiyo sasa kitakua chini ya makocha wa kikosi cha timu ya vijana ya klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala