Connect with us

Makala

Lawi Aiangukia Kamati TFF

Beki wa klabu ya Coastal union Lameck Lawi hatimaye amerejea nchini baada ya kushindwa kufuzu majaribio yake katika klabu ya K.A.Gent ya nchini Ubelgiji huku akisubiri uamuzi wa Kamati ya usajili na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la soka nchini (TFF).

Awali mchezaji huyo alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu katika klabu ya Simba sc baada ya klabu hiyo kufikia makubaliano na klabu yake ya Coastal Union na kutambulishwa kabisa lakini dili hilo liliingia mgogoro ambapo Klabu ya Coastal union ilidai kuwa Simba sc imekiuka baadhi ya makubaliano katika usajili huo na hivyo mchezaji huyo ataenda nchini Ubelgiji kujiunga na klabu ya Gent.

Mambo yalianza kwenda tofauti baada ya mchezaji huyo kutakiwa kufanya kwanza majaribio ambapo ilionekana kuwa hakukidhi vigezo vya kusajiliwa na timu ya vijana ya klabu hiyo baada ya kushindwa pia kusajiliwa timu ya wakubwa kutokana na kutokua na sifa zilizotakiwa na timu hiyo.

Huku pia hapa nchini baada ya mgogoro huo iliizimu klabu ya Simba sc kushtaki katika kamati ya usajili na hadhi za wachezaji TFF ambapo iliwaagiza klabu zote mbili kukaa na kukubaliana kuhusu usajili huo kabla ya kamati hiyo kuingilia endapo watashindwana.

Taarifa zinadai kuwa tayari timu hizo zimekutana na zimeshindwa kufikia muafaka ambapo kila klabu inataka ianze kufaidika na mauzo ya mchezaji huyo huku mwingine akipata pesa kidogo wakiwa na matarajio kuwa dili la kusajili Gent liko mbioni.

Kutokana na masuala hayo kwenda kinyume na matarajio sasa mchezaji kasharejea nchini na sasa inasubiri kamati hiyo kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu hatma ya usajili wa Lawi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala