Connect with us

Makala

Simba Sc Yaanza Ligi na 3G

Klabu ya Simba Sc imeanza ligi kwa gia kubwa baada ya kuizamisha Tabora United kwa mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex jijini Dar es Salaam.

Ikianza na kikosi chenye mabadiliko machache kutoka kile kilichocheza na Yanga sc na kupoteza moja bila ambapo beki Abdulrazak Hamza alichukua nafasi ya beki wa kigeni Chamou Karabou huku wengine wakibako wale wale.

Iliwachukua Simba Sc dakika 14 kushangalia bao la kwanza la msimu lililofungwa na Che Fondoh Malone akiunganisha kwa kichwa krosi safi ya Jean Charles Ahoua huku ikiwaazimu kusubiri mpaka dakika ya 69 kupata bao la pili lilifungwa na Valentino Mashaka ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Steven Mukwala na kufungwa  kwa kichwa akimalizia krosi ya Mohammed Hussein kutokea upande wa kushoto.

Awesu Awesu alimalizia furaha ya mabao kwa Wanasimba dakika 90+3 alipopiga shuti pembeni ya goli na mpira kujaa wavuni na kuandika bao la tatu lililoifanya Simba sc kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya soka ya Nbc.

Pamoja na ushindi hup Simba sc ilionyesha soka safi licha ya kukosa nafasi nyingi za wazi huku kukiwa na kukosekana kwa mawasiliano mazuri katika eneo la ufungaji.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala