Connect with us

Makala

Rasmi Awesu Asalia Simba Sc

Baada ya Mazungumzo ya muda mrefu hatimaye klabu za Simba Sc na Kmc zimefikia muafaka kuhusu usajili ya kiungo mshambuliaji Awesu Ali Awesu ambaye alisababisha timu hizo kuingia mgogoro wa usajili.

Awali Simba sc ilimtambulisha Awesu kuwa mchezaji wake mpya ikimsajili kama mchezaji huru baada ya kununua mkataba wake na waajiri wake Kmc kwa kulipa kiasi cha shilingi milioni hamsini zilizopo katika kipengele cha kuvunja mkataba wake.

Kmc iliamua kukimbilia katika kamati ya usajili na hadhi za wachezaji ambayo iliamua kumrejesha mchezaji huyo Kmc kutokana na kutofuata utaratibu wa kuishirikisha klabu katika kuvunja mkataba wake uliokua umesalia mwaka mmoja.

Baada ya suala hilo kuamuliwa na kamati hiyo ambapo ilimlazimu mchezaji kurejea Kmc huku Simba sc wakilazimika kufungua Mazungumzo upya ya kumsajili staa huyo aliyekua anahitajika na kocha Fadlu Davis kutokana na kuwepo katika mipango yake ya msimu ujao.

Simba sc na Kmc sasa zimefikia muafaka kuhusu usajili huo ambapo Simba sc sasa imelipa kiasi kinachokadiriwa kufikia shilingi milioni mia moja na tayari mchezaji huyo ameingizwa katika mfumo wa usajili wa klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala