Connect with us

Makala

Kibu Dennis Azua Maswali

Mpaka sasa staa wa klabu ya Simba sc Kibu Dennis hajaripoti kambini nchini Misri kuungana na mastaa wengine ambao wanajifua vilivyo chini ya kocha mpya Fadlu Davis ambaye ametua klabuni hapo msimu huu na sasa anatafuta kikosi cha kwanza kwa ajili ya msimu ujao.

Inasemekana kuwa staa huyo ana mgomo baridi unaotokana na kupata ofa mpya nchini Norway ambapo anatafuta namna ya kuwaingia mabosi wa klabu hiyo ili wamruhusu huku pia vyanzo vingine vikiripoti kuwa utoro huo unatokana na kutomaliziwa pesa ya usajili baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili hivi karibuni.

Kwa mujibu wa gazeti la michezo la Mwanaspoti ni kuwa Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimeliambia  staa huyo ambaye msimu uliopita alifunga bao moja katika ligi dhidi ya Yanga uwezekano wa kwenda Misri kuungana na wenzake ni mdogo, hivyo ana asilimia kubwa ya kuisubiri timu irudi Dar.

Kutokana na ishu hiyo, inaelezwa kuwa uongozi wa Simba unadaiwa kufikia uamuzi wa kumkata nusu mshahara kutokana na kushindwa kufika kambini kama ilivyotakiwa kwa nyota wote.

Hata hivyo endapo mpango huo wa kuondoka klabuni hapo usipofanikiwa staa huyo atakua na wakati mgumu kutokana na ukweli kwamba atakua na kazi ngumu kumshawishi mwalimu ambaye atakua tayari ameshapata kikosi cha kwanza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala