Klabu ya Azam Fc imefunga usajili wake kwa kumsajili kiungo Mamadou Samake ambaye ametokea katika miamba ya soka nchini Algeria CR Belouizdad ambapo amesajiliwa klabuni hapo kwa mkataba wa miaka miwili kuungana na mastaa wengine kurudisha makombe yaliyokaukwa Chamazi.
Azam Fc inastahili pongezi kubwa baada ya kuamua kununua mkataba wa staa huyo aliyezaliwa mwaka 2000 huku alikua akiviziwa na klabu kadhaa barani ulaya kama ilivyo kwa Cheikna Diakite ambaye nae ametua Chamazi akitokea Real Bamako Fc.

Usajili wa Samake unatajwa kuwa ni pendekezo la kocha Yousouph Dabo wa Azam Fc ambaye inaelezwa kuwa hajaridhishwa na kiwango cha James Akaminko kwa siku za hivi karibuni ambapo pia amekua na majeraha ya mara kwa mara huku viungo Sospeter Bajana na Yahaya Zayd anaopendelea kuwatumia nao wanasumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara huku Zayd akikosekana karibia nusu ya msimu kutokana na kufanyiwa upasuaji.
Tegemeo pekee la mwalimu Dabo lilikua na Adolf Bitegeko ambaye naye inaelezwa kuwa amegoma kusaini mkataba mpya baada huu alionao sasa kuelekea tamati ambapo unatarajiwa kumalizika Januari 2025 na inatajwa sababu kubwa wa kugomea kusaini ni kuwa na ofa nono ya Yanga sc.
Usajili ya Samake sio tu unawaimarisha Azam Fc bali pia unawatisha vigogo wa soka nchini Simba sc na Yanga sc kutokana na ukweli kuwa kiwango cha staa huyo ni kikubwa na aliwasumbua sana Yanga sc katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya CR Belouzdad na kuwafanya waambulie kipigo cha 3-0.