Connect with us

Makala

Lawi Azua Kizazaa TFF

Klabu ya Simba sc imefungua shauri katika kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la soka nchini (TFF) ikilalamikia klabu ya Coastal Union juu ya usajili wa mchezaji Lameck Lawi ambaye mpaka sasa klabu ya Coastal Union imekaa kumruhusu kujiunga na Simba sc.

Awali baada ya Simab sc kumtambulisha Lawi kama mmoja ya wachezaji iliowasajili msimu huu klabu ya Coastal ilikana kumuuza mchezaji huyo katika klabu ya Simba sc huku ikikiri kuwepo na makubaliano baina yao ambayo yalivunjika baada ya Simba sc kushindwa kulipa pesa kwa wakati na kusababisha Coastal Union kurejesha baadhi ya pesa ya awali iliyokua imelipwa na dili hilo kufa rasmi.

Klabu ya Coastal ilisisitiza kuwa baada ya dili hilo kufa tayari imepata dili jingine katika klabu ya Genk Fc ya nchini Ubelgiji na inajiandaa kumuuza mchezaji huyo huko baada ya klabu hiyo kuweka ofa nono kwa klabu na mchezaji mwenyewe.

Ofisa habari wa Coastal Union, Abbas El Sabri amesema, klabu hiyo imepokea wito wa kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya kusikiliza shauri la mchezaji wao Lameck Lawi ambalo limesikilizwa leo Julai 16, 2024 ambapo wameshindwa kufikia muafaka mpaka sasa.

“Bado uamuzi haujafikiwa Shauri tayari limesikilizwa na ndugu zetu wa Simba Sc wamewasilisha hoja zao ikiwa ndio utaratibu tuliokubaliana kumaliza suala hilo wakati tumefikia makubaliano ya suala hilo hivyo tuendelee kusubiri na hili sio suala la ushindi bali ni suala la kutafsiri Kanuni na Sheria na tunaamini kila mmoja haki yake atapewa”Alisema Katibu wa Coastal Union, Omary Ayub wakati akizungumza mara baada ya kutoka kwenye kamati ya katiba, Sheria na hadhi za wachezaji kuhusu suala la hilo.

Mpaka sasa mchezaji huyo pamoja na kutangazwa na Simba sc bado hajahudhuria mazoezi ya klabu hiyo akiendelea na mazoezi ya Coastal Union sambamba na kushughulikia safari yake ya kwenda nchini Ubelgiji.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala