Connect with us

Makala

Diarra Kukaa Jangwani mpaka 2027

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili kipa wake namba moja Djigui Diarra mpaka mwaka 2027 ikihofiwa kipa huyo kushawishiwa na klabu zingine.

Diarra alijiunga na Yanga sc mwaka 2021 akitokea Stade de Mallien ya nchini Mali ambapo amefanikiwa kuibadili Yanga sc katika mfumo mzima wa uchezaji ambapo imekua ikianzisha mashambulizi kuanzia nyuma.

Inasemekana Rais wa Yanga sc Eng.Hersi Said anamuona Diarra kama mtu muhimu katika ujenzi wa kikosi chake kutokana na kujua kuanzisha mashambulizi na kuituliza timu pindi inapokua inashambuliwa.

Mbali na Diarra mastaa wengine kama Stephane Aziz Ki,Bakari Mwamnyeto na Nickson Kibabage wameongeza mkataba wa kukaa klabuni hapo wakivutiwa hasa na maslahi pamoja na mafanikio ya kikosi hicho kwa siku za karibuni.

Msimu wa 2023/2024 kikosi hicho kiliweka rekodi ya kufanya vizuri zaidi katika historia ya klabu hiyo kikifanikiwa kutwaa mataji yote nchini pamoja kufika hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (Caf confederation cup).

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala