Connect with us

Makala

Kambole Aikomalia Yanga sc

Licha ya kulimaliza suala ya Mamadou Doumbia kwa kufanikisha kujaza taarifa za malipo ya usajili wa mchezaji huyo bado klabu ya Yanga sc imeendelea na kifungo cha kutosajili cha Shirikisho la soka duniani (Fifa) kutokana na kutokamilisha malipo ya mchezaji Lazarus Kambole.

Yanga sc iliachana na Kambole msimu mmoja pekee baada ya kumsajili kutokana na kutoridhishwa na uwezo wake lakini mchezaji huyo aliishitaki klabu hiyo Fifa kutokana na kutomaliziwa baadhi ya fedha za usajili na mishahara yake kipindi ambacho alitolewa kwa mkopo kwenda klabu ya Wakiso Giant ya nchini Uganda.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) imeonyesha kuwa klabu hiyo imeendelea na kifungo cha usajili wa ndani na wa kimataifa licha ya kukamilisha nyaraka zote za malipo ya usajili wa Doumbia katika mfumo wa usajili wa kimataifa (TMS).

Katazo hilo litaawaathiri Yanga sc kukamilisha baadhi ya sajili kutokana na kuhitaji kufanya maboresho ya kikosi chake kipindi hiki cha dirisha kubwa la usajili ambapo hawataweza kusajili majina ya wachezaji wapya na wale waliongeza mikataba katika mfumo huo wa usajili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala