Connect with us

Makala

Mbappe Atua Real Madrid

Mshambuliaji wa klabu ya Paris St.German Kylian Mbappe amejiunga na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania kwa dau la paundi 150 kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kugoma kuongeza mkataba katika klabu yake ya sasa ya Psg.

Mbappe alijunga na Psg mwaka 2017 akitokea Fc Monaco ambapo aligoma kujiunga na Real Madrid akiichagua Psg ambapo mwaka 2022 aligomea tena jaribio la Real Madrid kumsajili na kuamua kuongeza mkataba Psg ambapo sasa amekubaliana rasmi na Real Madrid kujiunga nao huku akipokea mshahara wa paundi 15 milioni kwa mwaka akiwa ndie staa ataekuwa analipwa zaidi akiwapita David Alaba anayepokea paundi 12.5 milioni na Luca Modric anayepokea paundi milioni 11.

Staa huyo ni kama amekubali kupunguza mshahara wake aliokua akiupokea katika klabu ya Psg huku pia akifaidika na dau la usajili ya paundi milioni 150 ambalo atapatiwa kwa mafungu katika miaka mitano ya mkataba wake na klabu hiyo huku akipokea mshahara na marupurupu manono baada ya kodi.

Licha ya kudumu nchini Ufaransa katika klabu ya Psg kwa miaka saba staa huyo aliongoza kwa ufungaji bora katika ligi kuu nchini humo kwa misimu sita mfululizo huku akishinda kila tuzo ya ndani na kubakisha kushinda tuzo ya mchezaji bora ya dunia na medali ya klabu bingwa barani ulaya ambapo anaamini ndoto hizo zitatimia.

Haikua rahisi kwa Mbappe kuachana na Psg ambapo mara kadhaa rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron alijitahidi kumshawishi staa huyo asiondoke klabuni hapo huku pia timu ya Al Hilal ya Saudia ilimuwekea kiasi kufuru cha pesa ajiunge na timu hiyo ambapo alimuwekea mshahara wa mnono na dau la usajili la paundi milioni 327 lakini staa huyo alikataa.

Msimu huu Mbappe amefunga jumla ya mabao 44 huku akifunga mabao 27 katika ligi kuu akichukua tuzo ya mfungaji bora mara ya sita mfululizo na anaenda kuungana na mastaa kama Vinicius Jr,Judde Bellingham na Rodyrigo Goes kuunda safu hatari ya ushambuliaji klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala