Kwa mujibu wa chanzo makini ndani ya klabu ya Simba Sc ni kuwa kuna mabadiliko makubwa yanakuja kiutawala klabuni hapo ambapo baadhi ya vigogo wataachia mgazi ili kuruhusu nguvu na mapya klabuni humo.
Kwa mujibu wa Taarifa za ndani ni kuwa Kamati mpya ya mashindano ya klabu ya Simba itakuwa chini ya Mwenyekiti, Crescentius Magori ambaye amewahi kuhudumu klabuni hapo enzi za Simba sc ya moto iliyofika robo fainali ya michuano ya Klabu bingwa barani Afrika ikiwafunga Nkana Fc na As Vita na kutolewa na Tp Mazembe.
Magoli tangu aondoke Simba sc amekua akijihusha na mambo mbalimbali yanayoohusu klabu hiyo ambapo amekua mshauri wa Rais wa heshima wa klabu hiyo Mohamed Dewji katika masuala mbalimbali yanayohusu klabu hiyo.
Kutokana na mwenendo wa kusuasua wa klabu hiyo ambapo hali hiyo imesababisha kuwapa nafasi Yanga sc kuongoza ligi kuu kwa tofauti ya alama tisa mpaka sasa japo Simba sc wana mchez0 mmoja mkononi huku wakielekea kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini kwa mara ya tatu mfululizo na mara ya 30 kwa ujumla wake.
Inasemekana kuwa tayari kikao cha maamuzi kilichofanyika siku chache zilizopita kimepitisha kuajiriwa kwa Afisa Mtendaji mkuu mpya klabuni hapo kuchukua nafasi ya Imani Kajula huku pia nafasi ya Salim Abdalah “Try Again” pia ikiwa hatarini kuchukuliwa na utawala mpya wenye lengo la kurudisha makali ya klabu hiyo ikiwemo kufanya usajili bora na makini.
Pia baadhi ya mastaa kama Saido Ntibanzokiza,Pa Omari Jobe,Kennedy Juma,Henock Inonga Baka,Shomari Kapombe,Fredy Michael nafasi zao ziko hatarini kutokana na mabosi wa klabu hiyo kuamua kuanza kutafuta mbadala wao katika nafasi hizo.