Connect with us

Soka

Nzengeli Kuikosa Namungo Fc

Kikosi cha klabu ya Yanga sc kimewasili mkoani Mtwara mapema mchana wa leo kwa ndege ya kukodi tayari kwa mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Nbc dhidi ya Namungo Fc utakaofanyika katika uwanja wa Majaliwa wilayani Ruangwa.

Kikosi hicho kikiwasili kocha Miguel Gamondi amethibitisha kukosekana kwa kiungo Maxi Nzengeli kutokana na kuwa majeruhi ambapo aliumia siku ya mchezo wa kufuzu robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Cr Belouzdad uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

“Siwezi kuacha kumtumia Nzengeli (Maxi) bila sababu ni mchezaji mzuri na ana mchango mkubwa kwa timu hakutumika kwa sababu ni majeruhi na bado anaendelea na matibabu alipata shida kwenye mkono uliofungwa POP,”Alisema Gamond akiongea na waandishi wa habari.

Max amekua na mchango mkubwa klabuni hapo ambapo mpaka sasa katika ligi kuu ya Nbc ameifunga klabu hiyo jumla ya mabao nane akiwa katika namba tatu ya orodha ya wafungaji bora wa ligi kuu msimu huu ambapo mpaka sasa timu yake imecheza jumla ya michezo 16 tu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka