Connect with us

Soka

Simba Sc Yazoa Alama Tatu Jioni

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuchukua alama tatu baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Geita Gold Sc katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.

Kocha Dennis Kitambi alifanya utafiti wa kutosha kuhusu mbinu za Kocha Abdelhack Benchika kiasi cha kufanikiwa kuziba mianya yote huku akiwazuia vizuri viungo wa Simba sc wakiongozwa na Fabrice Ngoma na Mzamiru Yassin ambao hawakupata nafasi ya kutoa pasi za mwisho kwa Pa Omar Jobe.

Kocha Benchika alifanya mabadiliko kadhaa ambayo yalizaa matunda hasa baada ya kuingia Luis Miquisone na Babacar Sarr ambao walitengeneza bao la pekee katika mchezo huo baada ya Miqquisone kupiga pasi ndefu na Kibu Dennis kumtengea Sarr dakika ya 82 ambaye alifunga bao lbaada ya mpira kumshinda  kipa wa Geita Gold Fc Costantine ambaye alifanya kazi kubwa tangu mwanzo wa mchezo.

Simba sc sasa imecheza jumla ya michezo 14 ikiwa na alama 33 katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu huku Yanga sc wakiwa kileleni mwa msimamo na alama 40 katika nafasi ya kwanza baada ya michezo 15 ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka