Connect with us

Soka

Azam Fc Kuwakosa Wanne

Kocha wa Azam FC, Bruno Ferry amesema kikosi chake kitawakosa wachezaji wanne kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Simba katika Ligi Kuu Bara, huku akiwatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kusema kikosi chake kimejiandaa vizuri na ni kipana kinachoweza kupambana na kupata ushindi.

Azam itakuwa mgeni wa Simba kesho kuanzia saa 10 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ambapo mastaa watakaokosekana ni Sospeter Bajana, Abdallah Heri ‘Sebo’, Malickou Ndoye na mshambuliaji Alassane Diao.

Ferry amesema mchezo huo utakuwa mgumu kwa kuwa wanakutana na timu bora yenye benchi la ufundi linaloongozwa na kocha mwenye wasifu mkubwa Afrika, lakini na wao wamejiandaa vya kutosha, huku akitahadharisha na kutaka marefa wachezeshe kwa haki na atakayepata ushindi uwe sahihi.

“Utakuwa mchezo wenye presha, lakini tunahitaji uamuzi sahihi kwa timu zote. Hatuhitaji kushindwa ama kushinda kwa sababu ya uamuzi usio sahihi kwa hiyo tunaomba marefa watende haki. Itakuwa ni mapambano na wachezaji wako tayari kupambana, tunafahamu ni mchezo wa presha lakini tumemudu kuipunguza.”

“Tumejiandaa vizuri kwa siku chache zilizopita na tutegemee wachezaji wapya kuonekana kesho, japo wanazoea taratibu mazingira wanahitaji kuchukua muda, lakini kimwili na kisaikolojia wako tayari kwa mchezo na kuisaidia timu. Tuna wachezaji wa daraja la juu na benchi la ufundi bora kwa hiyo tuko tayari.”

Mchezo huo utakua mgumu kwa timu zote kutokana na timu hizo kuhitaji matokeo ya ushindi ili kukaa juu ya msimamo wa ligi kuu nchini ambapo Yanga sc ipo kileleni ikiwa na alama 37 huku Azam Fc ikiwa na alama 31 katika nafasi ya pili na Simba sc ipo nafasi ya tatu na alama 29 ikiwa na michezo miwili mkononi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka