Connect with us

Soka

Yanga Sc Yazindua Ofisi

Klabu ya Yanga sc imekamilisha ukarabati wa ofisi za klabu hiyo zilizopo katika mitaaya Twiga na Jangwana na kuhamia rasmi katika jengo hilo lililojengwa miaka ya 50 na waasisi wa klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1935.

Awali klabu hiyo ilikua ikitumia jengo la Salamander Tower lililopo Posta jijini Dar es salaam ambapo walipewa hifadhi na kampuni ya Gsm ambao ndio wamiliki wa jengo hilo la kisasa.

Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo alikua ni Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Hamis Mwinjuma ambaye alitembelea ofisi hizo baada ya kukata utepe kuzizindua ofisi hizo ambapo alisema kuwa Rais Samia ameridhia mradi ambao Yanga sc itanufaika kwa kupata eneo la kujenga uwanja.

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameridhiria marekebisho ya mto Msimbazi kupitia benki ya dunia, ambapo kutakuwa na mradi mkubwa wa maendeleo katika eneo la Jangwani. Mradi huu utakaofanikisha Klabu ya Yanga kupata eneo lao kutengeneza uwanja wao”Alisema.

Pia Rais wa klabu ya Yanga sc Injinia Hersi Said alisema kuwa wao kama Yanga sc wanaishukuru kampuni ya Gsm kwa kuwahifadhi kwa takribani miaka mitatu na sasa shughuli rasmi zimehamia hapo Jangwani.

“Nisiwe mchoyo wa fadhila kwa mfadhili na mdhamini wetu Ghalib Said Mohamed(GSM) kwa kutupa hifadhi ya kiofisi kwenye jengo lake kabla ya kufanikisha maboresho ya ofisi zetu. Mr Ghalib alifanya kwa nafasi yake kwa kutuhudumia kwa miaka mitatu, sasa ni wajibu wa Wanachama wa Klabu hii kuhakikisha kuwa ofisi hizi za Jangwani zitaendelea kuimarika na kuwa bora kwa matumizi. Wanachama wa Klabu hii wanaalikwa kuja kuhudumiwa katika ofisi hizi muda wote”Alisema Hersi

Yanga sc imeendelea kufanya vizuri ndani na nje ya uwanja ambapo mpaka sasa ipo kileleni mwa ligi kuu nchini na huku ikiendelea na usajili wa wanachama ili kuongeza kipato katika kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka