Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na alama tatu baada ya kuifunga Medeama Fc kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kombe la klabu bingwa barani Afrika uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.
Mchezo wa nne kwa timu hizo katika kundi D la michuano hiyo unaifanya Yanga sc sasa kufikisha alama tano katika nafasi ya pili ya msimamo wa kundi hilo huku Medeama Fc wakisaliwa na alama nne katika michuano hiyo.
Yanga sc ikianza na kikosi kile kile kilichoanza katika mchezo wa kwanza nchini Ghana isipokua Kennedy Musonda na Mudathir Yahaya ambao walichukua nafasi ya Ibrahim Hamad na Clement Mzize ambao walianzia benchi huku Medeama Fc wakiingiza full kikosi kikiongozwa na mshambuliaji wao maarufu Jonathan Sowah.
Iliwalazimu Wananchi kusubiri mpaka dakika ya kusubiri Mpaka dakika ya 33 ya kipindi cha kwanza kupata bao la uongozi kutoka kwa Pacome Zouzou aliwatoka walinzi wa Medeama Fc na kufumua shuti kali lililomshinda kipa wa Felix Kyei.
Yanga sc inabidi wajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuondoka na ushindi mnono ambapo washambuliaji wa timu hiyo wakiongozwa na Kennedy Musonda walikosa nafasi nyingi za wazi ambapo dakika ya 61 kichwa cha Musonda kilimgonga Bakari Mwamnyeto na kuipatia Yanga sc bao la tatu huku shukran ziende kwa Kipa Djigui Diarra kwa kucheza penati ya Jonathan Sowah.
Mudathir Yahaya alipokea pasi nzuri kutoka kwa Aziz Ki baada ya mabeki wa Medeama Fc kupoteza mpira kizembe na kufunga bao la tatu kwa Yanga sc dakika ya 66 ya mchezo.
Kocha Miguel Gamondi baada ya kuongoza kwa mabao 3-0 alifanya mabadiliko akiwaingiza Hafidh Konkoni,Mahlatse Makudubela,Salum Abubakar kuja kuongeza nguvu ili kulinda ushindi huo ambapo mpaka dakika 90 zinatamatika Yanga sc aliibuka na alama tatu na kujitengenezea mazingira mazuri ya kufuzu robo fainali kwa mara ya kwanza.