Connect with us

Soka

Yanga sc Yanasa Kiungo Zanzibar

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuinasa saini ya kiungo wa JKU ya Zanzibar  Shekhan Ibrahim Khamis (18) kwa mkataba wa miaka mitatu ikiwazidi kete klabu za Simba sc na Coastal Union ambazo nazo zilikua zinamnyemelea kinda huyo.

Kiungo ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi za kiungo mkabaji na mshambuliaji huku akiwa na uzoefu wa kuitumikia klabu yake ya JKU na timu ya taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 18.

Licha ya kiungo huyo kutangulia kuzungumza na Simba sc lakini uwepo wa Arafat Haji makamu wa Rais wa Yanga sc ambae kikazi yupo Zanzibar alifanikisha usajili wa kiungo huyo baada ya kupata pendekezo la kocha Miguel Gamondi ambaye alimuona nchini Kenya katika michuano ya Cecafa ya vijana chini ya miaka 18.

Shekhan atakua na kazi kubwa ya kuwania namba kutoka kwa viungo wakongwe wa Yanga sc Khalid Aucho,Mudathir Yahaya,Salum Abubakar na Jonas Mkude kutokana na viungo hao kuwa bora kikosini humo licha ya mwalimu Gamondi kutowatumia mara kwa mara.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka