Connect with us

Soka

Azam Fc,Gor Mahia Yahairishwa

Klabu ya Azam Fc imetangaza kutokuwepo kwa mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Gormahia Fc uliokua ufanyike nchini Kenya siku ya Jumapili Novemba 19 kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa timu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa za awali ilibidi klabu hiyo isafiri kuelekea nchini humo kwa ajili ya mchezo huo lakini kutokana na hilo sasa mchezo huo hautakuwepo na badala yake sasa timu hiyo itaacheza na Jku siku ya Jumapili katika uwanja wa Azam Complex chamazi.

“Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia uliotakiwa kufanyika Jumapili hii nchini Kenya, sasa haupo tena”.Ilisomeka taarifa iliyochapishwa katika mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.

“Baada ya kushindikana kwa mchezo huo, hivi sasa kikosi chetu kitacheza dhidi ya JKU ya Zanzibar, utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex keshokutwa Jumapili saa 1.00 usiku”.Ilimalizia taarifa hiyo.

Baada ya ligi kuu kusimama kupisha kalenda ya Fifa ya mechi za kimataifa klabu hiyo haikutana kupoteza utimamu wa mechi wa wachezaji wake ndio maana imeaandaa michezo hiyo ya kirafiki.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka