Klabu ya Simba sc sasa ipo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jioni ya Oktoba 5 2023.
Simba sc ilianza langoni ikiwa na Ally Salim aliyechukua nafasi ya Ayoub Lakred huku Shomari Kapombe na Mohamed Hussein wakisaidiana na Che Malone na Kennedy Juma kuunda safu ya ulinzi na Mzamiru Yassin,Chama,Ngoma pamoja na Saido Ntibanzokiza wakiunda safu ya kiungo ya timu na John Bocco pamoja na Kibu Dennis wakiunda safu ya ushambuliaji.
Tanzania Prisons wakiingia na kikosi cha kile kile cha mara kwa mara walifanikiwa kupata bao la mapema dakika ya 12 kupitia kwa Edwin Balua lakini bao hilo halikudumu baada ya Cletous Chama kusawazisha dakika ya 34 na John Bocco alifunga bao la pili kwa Simba sc mwishoni mwa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kila timu ilipanga mashambuliz yake vizuri huku kukiwa na kosa kosa za hapa na pale lakini mwamuzi aliizawadia Simba sc penati dakika ya 86 ambapo Saido Ntbanzokiza alifunga na kuipatia Simba sc bao la tatu na mpaka mchezo unakwisha matokeo yalibaki 3-1.
Kutokana na matokeo hayo Simba sc sasa imejikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikiwa na alama 12 baada ya kushinda mechi zote nne huku Azam Fc ikiwa katika nafasi ya pili ikiwa na alama 1o na Yanga sc wakiwa nafasi ya tatu na alama 9.
Tanzania Prisons baada ya kupoteza mchezo huo sasa wamebakiwa na alama 1 wakiwa katika nafasi ya mwisho ya msimamo wa ligi kuu ya soka nchini.