Connect with us

Makala

Hapatoshi Namungo Ikiwasili Kagera

Klabu ya Namungo Fc maarufu kama Wauaji wa Kusini  tayari wamewasili mjini Bukoba kwa ajili ya mchezo dhidi ya Kagera sugar utakaopigwa uwanja wa kaitaba siku ya Jumatano Oktoba 4,2023.

Namungo wamewasili mkoani humo kwa ndege wakiwa na mastaa wote hasa wale waliocheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga sc walipofungwa 1-0 licha ya kufanikiwa kucheza vizuri mchezo huo na kutoa ushindani wa kutosha kwa mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini.

Namungo Fc wanapaswa kushinda mchezo huo ili kujikwamua kutoka mkiani ambapo mpaka sasa wana alama mbili pekee baada ya kupata sare mbili na kufungwa michezo miwili kati ya minne ya ligi kuu mpaka sasa huku Kagera Sugar wakiwa na alama nne katika michezo minne ya ligi kuu.

Katika michezo ya mwisho Kagera Sugar walipata sare dhidi ya Jkt Tanzania huku Namungo Fc wakipata suluhu nyumbani dhidi ya Mashujaa Fc ya Kigoma.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala