Connect with us

Makala

Tape Aondoka Azam Fc

Uongozi wa klab ya Azam na Mchezaji wao Tape Edinho wamefikia makubaliano ya pande zote mbili Juu ya kuvunja mkataba uliosalia wa mwaka mmoja wa staa huyo raia wa Ivory Coast.

Tape amelipwa Stahiki zake zote na  kupewa baraka za kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine baada ya kocha Yousuph Dabo kujiridhisha kuwa hana mpango nae baada ya kukaa nae siku kadhaa katika kambi ya klabu hiyo nchini Tunisia.

Pia kutemwa kwa mchezaji huyo kumechangiwa na kuzidisha idadi ya wachezaji wa kigeni ambao kwa mujibu wa kanuni wanapaswa kuwa 12 pekee ambapo klabu hiyo ilikua nao jumla 14.

Tape alisajiliwa msimu uliopita pamoja na Kipre Jr ambapo baada ya nusu msimu alitolewa kwa mkopo kunako klabu yake ya zamani nchini Ivory Coast ya Stella Club d’Adjameambapo alikaa kwa kipindi cha miezi sita na kisha kurejea klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala