Connect with us

Makala

Winga Kiberenge Anukia Yanga sc

Klabu ya Yanga sc wapo katika hatua nzuri za mazungumzo ya kumsajili winga raia wa Ivory Coast Aubin Kramo Kouame ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Asec Mimosas inayoshiriki ligi kuu  nchini humo,

Kramo mwenye umri wa miaka 27 anatumia zaidi mguu wa kushoto huku akiwa anamudu vyema kucheza winga zote za kulia na kushoto ambapo msimu uliopita alifanikiwa kuifungia timu hiyo mabao tisa na kutoa pasi nane za mabao.

Chanzo kutoka nchini Ivory Coast kimeeleza kuwa Yanga s wapo katika mazungumzo ya kumsajili winga huyo ambaye ni moja kati ya wachezaji bora ndani ya Ligi kuu ya Ivory Coast ili kuziba nafasi ya Tuisila Kisinda ambaye amerudi katika klabu yake ya Rs Berkane baada ya mkataba wake wa mkopo kuisha.

Yanga sc inamsajili winga huyo ili kuboresha mashambulizi kutokea pembeni ikiwa tayari imembakisha Jesus Moloko huku sasa ikitafuta winga kuja kuziba pia nafasi ya Benard Morrison ambaye ina mpango wa kuachana nae.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala