Connect with us

Makala

Hatimaye Yanga sc Yawasili Singida

Baada ya jana kushindwa kutua jijini Dodoma kwa ndege na kulazimika kurudi jijini Dar es salaam usiku na kusafiri tena mapema asubuhi ya leo,Hatimaye kikosi cha klabu ya Yanga sc kimefanikiwa kuwasili mkoani Singida kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars.

Yanga sc ilikwama jana jijini Dodoma baada ya kutokea hitilafu katika mfumo wa taa za ndege uwanjani hapo na kuilazimu ndege kushindwa kutua na kurejea jijini Dar es salaam na leo asubuhi kikosi hicho kilifanikiwa kufika salama mkoani Dodoma kisha kupanda basi la timu na kuelekea mkoani Singida kwa ajili ya mchezo huo utakaofanyika siku ya Alhamis Mei 4.

Yanga sc itakua na kibarua kigumu mbele ya wenyeji wanaotaka kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-1 katika mchezo wa awali jijini Dar es salaam pia ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu michuano ya kimataifa msimu ujao ambapo Tanzania tupo katika nafasi ya kuingiza timu nne.

Katika msimamo wa ligi kuu Yanga sc wapo kileleni wakiwa na alama 68 katika michezo 26 ya ligi kuu inayodhaminiwa na benki ya Nbc huku Singida Big Stars wakiwa na alama 51 baada ya kucheza michezo 26 katika nafasi ya nne ya msimamo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala