Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kuifunga Uganda katika mchezo wa makundi ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Ivory Coast na kufufua matumaini ya kufuzu kupitia kundi F.
Algeria iko katika nafasi ya kwanza ya msimamo wa kundi hilo ikiwa na alama tisa huku Taifa Stars ikiwa katika nafasi ya pili ya msimamo wa kundi hilo na alama nne huku Niger ikiwa na alama 2 na Uganda baada ya kupoteza mchezo huo sasa imefikisha alama 1 mkiani mwa kundi hilo.
Katika mchezo huo uliofanyika nchini Misri baada ya Uganda kukosa uwanja wenye hadhi ya Caf hivyo mchezo huo kufahamika nchini humo na Stars ikiongozwa na mwalimu Adel Amrouche ikiwa ni mchezo wake wa kwanza ilifanikiwa kupata bao dakika ya 68 likifungwa na Simon Msuva alikimalizia kazi nzuri ya Dickson Job aliyepiga krosi baada ya kupata pasi ya Mzamiru Yassin.
Ugamba ambayo ilianza na mkongwe Emmanuel Okwi katika eneo la mbele akisaidiwa na Bayo na Farouk Miya ambao walishindwa kupenya katika beki iliyoongozwa na Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca na Dickson Job huku Himid Mao na Mzamiru Yassin wakiweka ulinzi wa kutosha eneo la kiungo kumzuia Khalid Aucho asipige pasi za kwenda mbele.
Timu hizo zitarudiana tena wiki ijayo Machi 28 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam ambapo ili Stars ipate uhakika wa kufuzu inahitaji kushinda michezo miwili ijayo klabu ya kuwavaa Algeria ugenini.