Connect with us

Makala

Simba sc Yanukia Mapesa

Klabu ya Simba sc wamesaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya TSh 500 milioni na kampuni ya MobiAd Afrika inayojihusisha na miito ya kwenye simu za mkononi na masoko kwa ajili ya timu zao za vijana.

Mkataba huo umesainiwa mapema hivi leo mbele ya waandishi wa habari ambapo Mwenyekiti wa Bodi, Salim Muhene,Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Iman Kajula na wachezaji wa timu kubwa wakiongozwa na nahodha John Bocco sambamba na makocha wa timu za vijana za klabu hiyo walihudhuria utiaji saini wa mkataba huo.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Mwenyekiti wa bodi Salim Abdalah alikua na hasa ya kusema “Tuna malengo ya kuboresha soka la vijana, shamba ambalo tunajua litatusaidia kuvuna vipaji kwa ajili ya timu ya wakubwa. Tulikuwa tunaongea na mwekezaji wetu, ndugu Dewji amekubali kusaidia kuendeleza soka la vijana. Hivi karibuni tutaanza ujenzi wa kituo chetu.”

“Jambo hili lina neema kubwa. Niwashukuru MobiAd kwa kukubali kudhamini timu yetu ya vijana. Kama Simba Sports Club tunawaahidi kwamba fedha hizi zitatumika vizuri kwani vijana ndio msingi wa timu yetu.”Alisema Muhene maarufu kama Try Again.

Kwa upande wa kampuni hiyo wao walisema kuwa wanaamini vijana ndio nguzo ya maendeleo ya soka na ndio maana wameamua kuwekeza “MobAd tunaamini vijana wana mchango mkubwa kwa taifa. Tunaamini mpira wa miguu ni sehemu ya suluhisho la ajira kwa vijana. Simba ni timu kubwa Afrika na inazidi kuwa kubwa hivyo ni vizuri kuandaa vijana ambao watachukua nafasi ya hawa wa sasa.”Akisema mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Rumisho Shikonyi.

Simba sc sasa imekua ni timu pekee nchini ambayo ina udhamini wa kampuni tatu tofauti katika timu zake zote ikiwemo ya wanaume(M-bet),vijana(MobAd Africa) na wanawake (Africarriers).

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala