Connect with us

Makala

Yanga sc Yamweka Matatani Mwamuzi

Kufuatia kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold siku ya Jumamosi kufuatia bao la penati ambayo mwamuzi Florentina Zablon ameingia matatani kutokana na wadau wengi wa soka wakiwemo mashabiki na waandishi wa habari kulalamika wakionekana kutofurahishwa na kiwango cha mwamuzi huyo huku akigeuka mjadala katika mitandao ya kijamii.

Mwamuzi huyo alishindwa kutafasiri vizuri mpira wa kushikwa uliopigwa na Heritier Makambo ambapo ulimgonga beki ya Geita Gold Fc mkononi akiwa nje ya eneo la 18 lakini mwamuzi huyo aliweka penati na kuzua malalamiko kwa wachezaji wa Geita Gold Fc ambao waliishia kupata kadi za njano kutokana na kumzonga mwamuzi huyo.

Penati iliyopigwa na Benard Morrison ilijaa wavuni na kuandikia Yanga sc bao pekee la mchezo huo ambapo baada ya filimbi ya mwisho tukio hilo liligeuka mjadala mkubwa huku baadhi wakimlaumu mwamuzi na wengine wakihusisha na rushwa kuwa ndio imesababisha mwamuzi huyo kuipatia upendeleo Yanga sc.

Msemaji wa zamani wa klabu ya Yanga sc Hassan Bumbuli alikua na maoni yafuatayo kuhusu mwamuzi huyo ambayo aliyaandika katika mitandao wake wa kijamii wa Instagram “Florentina Zablon Sijui ni kwa maslahi gani huyu mama bado anachezesha Ligi Kuu? Nakumbuka baada ya mechi ya Disemba 24, 2019 Mbeya City vs Yanga huyu aliitwa mwamuzi Kichefuchefu kutokana na maamuzi yake ya hovyo kwenye mchezo huo uliomalizika kwa 0-0.

Baada ya hapo Yanga walimkataa kwa barua na sikumbuki kuichezesha tena Yanga hadi nilipomuona jana. Mechi zake kadhaa zimegubikwa maamuzi ya utata,Kuna namna ambayo tunapaswa kuboresha eneo hili la uamuzi, ili kutoa thamani halisi ya uwekezaji kwenye soka letu”

Ni dhahiri kutokana na mwamuzi huyo kushindwa kutafsiri sheria hiyo ataadhibiwa na bodi ya ligi ambapo anaweza kusimamishwa kushiriki michezo kadhaa kutokana na kamati ya ligi kuu itakavyojiridhisha.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala