Connect with us

Makala

Yanga sc Kuingia Sudan Kibabe

Klabu ya Yanga sc imepanga kutua nchini Sudan masaa 24 kabla ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya Al Hilal Fc ya nchini humo siku ya Jumapili Oktoba 16 katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wenye kuteka hisia za mashabiki wengi hapa nchini.

Yanga sc inatarajiwa kuondoka siku ya Jumamosi Alfajiri saa 10 ambapo itatua nchini Sudan saa sita mchana na moja kwa moja baada ya mapumziko mafupi itatua uwanjani kwa ajili ya mazoezi na ukaguzi wa uwanja kabla ya kesho yake kucheza mchezo huo ambapo ili Yanga sc wafuzu wanahitaji kupata ushindi ama sare ya kuanzia mabao 2 na kuendelea.

Tayari baadhi ya viongozi wa klabu hiyo wamewasili nchini humo kuweka mazingira sawa kwa ajili ya mapokezi ya timu hiyo itakapowasili ambapo msafara wenye watu wanaokadiriwa 80 utaingia nchini humo wakiwemo wachezaji 25 na viongozi 12 pamoja na mashabiki wachache kwa ajili ya kuongeza nguvu kikosini humo.

Yanga sc inapambana ili kuingia hatua ya makundi ya ligi ya klabu bingwa barani Afrika ambapo mara ya mwisho iliingia mwaka 1998 huku kwa miaka ya karibuni ikifanikiwa kuingia hatua ya makundi ya kombe la shirikisho mwaka 2015 na 2017.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala