Connect with us

Makala

Yanga sc Wajipange

Klabu ya Yanga sc haina budi kujipanga vya kutosha inapoelekea nchini Sudan kuvaana na timu ya Al Hilal Ormdouman ya nchini humo mchezo wa marudiano wa michuano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya awali siku ya Jumamosi kulazimishwa sare ya 1-1 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo Yanga sc ilipata bao dakika ya 52 ya kipindi cha pili likifungwa na Fiston Mayele akipokea pasi ya Khalid Aucho bao ambalo liliwapa matumaini Yanga sc lakini matumaini hayo yalizimwa na Mohamed Yousef aliyefunga bao dakika ya 68 baada ya kufanya shambulizi la kushtukiza langoni mwa Yanga sc na beki Dickson Job kuchelewa kuondosha mpira uliokua unazagaa na kumkuta mfungaji.

Baada ya bao hilo timu zote mbili ziliamua kujilipua na kuanza kushambulia ambapo zilikosa nafasi za wazi kwa pande zote mbili huku mpaka mwamuzi anapuliza filimbi ya mwisho mchezo ulikua 1-1 na kuipa kazi Yanga sc ya kupanda mlima mkubwa zaidi nchini Sudan katika mchezo wa marudiano.

Yanga sc inatakiwa kwanza ijipange kisaikolojia kukabiliana na vurugu za mashabiki wa klabu hiyo ambao hushangilia mwanzo mwisho kuisapoti timu yao kwa ngoma na kuwasha miale ya moto hali inayoweza kuwasumbua zaidi wachezaji wa Yanga sc kwani wanatakiwa kupata bao la mapema ili kuweza kuweka mizani sawa kama walivyopata Al Hilal hapa ugenini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala