Connect with us

Makala

Simba sc Kukodi Pipa

Klabu ya Simba sc imepanga kukodi ndege kuelekea nchini Angola katika mchezo wa ligi ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya klabu Premiero De Augosto wa raundi ya pili ya michuano ya hiyo mikubwa kwa ngazi za vilabu barani Afrika.

Simba sc imepanga kuingia nchini humo masaa machache kabla ya mchezo na baada ya mchezo kuwahi kurudi nyumbani mapema kujiandaa na mchezo wa marudiano hapa nchini baada ya wiki moja huku pia ikilazimika kutumia usafiri huo kupunguza hujuma zitakazotokana na kukaa muda mrefu nchini humo.

Simba sc imeingia katika hatua ya pili ya michuano hiyo ikifanikiwa kuitoa timu ya Nyassa Big Bullets ya nchini Malawa kwa jumla ya ushindi wa mabao 4-0 ikishinda mabao 2 kote ugenini na nyumbani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala