Connect with us

Makala

Zoran Aondoka Simba sc

Klabu ya Simba sc imetangaza kuachana na kocha wake Zoran Maki ikiwa ni takribani miezi miwili tangu ajiunge na klabu hiyo kama kocha mkuu kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Zoran ambaye ameiongoza Simba sc katika mechi rasmi moja tu ya ngao ya jamii dhidi ya Yanga sc akipoteza kwa mabao 2-1 anaondoka klabuni hapo pamoja na wasaidizi wake kocha wa viungo Sbai Karim na kocha wa makipa Mohamed Rachid ambao walijunga nae wakiwa kambini nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinadai kuwa kocha huyo ameomba kuondoka mwenyewe baada ya kupata ofa kutoka klabu ya Al Ittihad inayoshiriki ligi kuu nchini Misri ambapo klabu hiyo imeweka dau kubwa ambalo limewashawishi makocha hao kuondoka huku pia kukiwa na sababu zingine ambazo kocha huyo aliona ni bora kuondoka.

Simba sc baada ya kuachana na Maki tayari wapo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mwingine wa kuchukua nafasi ya Maki huku kwa sasa timu itakua chini ya uangalizi wa Seleman Matola kwa kipindi cha muda mfupi na kocha mpya atakuja mapema kuwahi michuano ya Caf ambayo Matola hana leseni hivyo hawezi kukaa benchi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala