Connect with us

Makala

Okrah Atua Simba sc

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Augustine Okrah kutoka klabu ya Benchem Fc inayoshiriki ligi kuu nchini Ghana ambapo Staa huyo tayari ametambulishwa klabuni hapo baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kukupiga hapo.

Okrah ambaye wadau wengi wa soka nchini Ghana hawakutarajia kama atakuja Tanzania badala ya kwenda mataifa yaliyoendelea zaidi kisoka hasa barani ulaya amewasili nchini na kukamilisha taratibu za kimkataba na sasa ni mali ya Simba sc kwa miaka miwili ijayo.

Msimu huu wa ligi kuu staa huyo amehusika katika upatikanaji wa  mabao  17 akiwa na Bechem ambapo amefunga 14 na kutoa pasi (Assisti) tatu katika michezo 31 aliyocheza huku akitarajiwa kuungana na kikosi hicho kinachoelekea Misri kesho kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Pamoja na Okrah pia klabu ya Simba sc tayari imekamilisha usajili wa Nassoro Kapama na Habib Kyombo huku pia ikisemekana tayari ilishamalizana na mastaa Cezar Manzoki na kiungo kutoka Rivers United ya Nigeria.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala