Connect with us

Makala

Pogba Kuondoka Man Utd

Kiungo Paul Pogba imethibitika ataondoka katika klabu ya Manchester United mwishoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake kumalizika ambapo inatajwa kuwa tayari yuko kwenye mazungumzo ya kujiunga na Juventus ama Paris st.Germans ya nchini Ufaransa.

Pogba alijiunga na Man utd akitokea Juventus mwaka 2016 miaka minne tangu aondoke Man utd kama mchezaji huru huku akirudi klabuni hapo kwa dau la rekodi ya usajili ya Paundi milioni 89 na sasa ataondoka tena kwa mara ya pili akiwa huru huku tayari Man utd imeanza mazungumzo ya awali kumsajili Frankie De Jong wa Barcelona kuchukua nafasi hiyo.

”Klabu inatangaza kwamba Paul Pogba ataondoka klabuni ifikapo mwezi juni ikiwa ni mwisho wa mkataba wake,kila mtu klabuni hapa anamshukuru Paul kwa mafanikio yake kwa Manchester United”.

Mshindi huyo wa kombe la dunia akiwa na timu ya Taifa ya Ufaransa mwaka 2018 anaondoka United ambako amekaa kwa miaka sita huku akishindwa kupata mafanikio makubwa kiwanjani na inatarajiwa anaweza kurudi Juventus ama kujiunga na Real Madrid na Psg japo kwa sasa yupo mapumziko Miami Marekani na anatarajiwa kufanya maamuzi hivi karibuni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala