Connect with us

Makala

Ki Aziz Kumrithi Saido Yanga sc

Klabu ya Yanga sc imeelekeza nguvu kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Asec Mimosa Aziz Ki ili kujiunga na klabu hiyo kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Saido Ntibanzokiza ambaye wameamua kuachana nae baada ya kushindwana katika vipengele vya mkataba mpya klabuni hapo.

Inasemekana baada ya kuachana na Saido tayari uongozi wa klabu hiyo umeanza mawasiliano na wakala wa Ki ambaye pia ndiye wakala wa Yacouba Songne aliyepo klabuni hapo.

Yanga sc ni moja ya timu ambazo zitashiriki michuano ya kimataifa msimu ujao hivyo inalengo la kutengeneza timu ya kuweza kushindana katika mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika ambapo kutokana na msimamo wa ligi kuu nchini Yanga sc ina nafasi kubwa ya kucheza michuano ya klabu bingwa.

Hata hivyo klabu hiyo inakabiliwa na ushindani mkubwa kumsajili Ki ambapo baadhi ya timu za Afrika Magharibi na ulaya zinamvizia mchezaji huyo aliyefunga mabao ya kuvutia katika kombe la shirikisho huku pia akiwafunga Simba sc mara mbili walipokutana katika michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala