Connect with us

Soka

Simba sc Yazoa alama 3 Tanga

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuchukua alama tatu katika mchezo muhimu wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union uliofanyika jijini Tanga baada ya kuifunga kwa jumla ya magoli 2-1 katika dakika tisini za mchezo.

Ikianza mpira kwa kuwatumia Chris Mugalu,Benard Morrison na Kibu Dennis,Simba sc ilifanikiwa kupata bao dakika ya 39 kwa juhudi binafsi akiuwahi mpira uliomgonga na kumchungulia kipa Musa Mbise na kuandika bao la uongozi lililodumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili Coastal waliamka na kushambulia kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 76 likifungwa na Victor Patrick Akpan ambaye aliuchopu mpira uliojaa nyavuni na kumshinda kipa Aishi Manula lakini Meddie Kagere alisawazisha dakika tatu za nyongeza baada ya tisini kuisha na kuipa alama tatu Simba sc.

Simba sc sasa imefikisha alama 40 ikiwa katika nafasi ya pili ya msimamo na itawavaa Polisi Tanzania siku ya Jumapili ikiwa ni mchezo wa kiporo utakaofanyika mkoani Moshi katika uwanja wa Ushirika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka