Ndivyo unavyoweza kusema kwa sasa kufuatia kocha wa klabu ya Yanga sc Nasredine Nabi kukiongoza kikosi cha klabu ya Yanga sc kwa mafanikio makubwa tofauti na ilivyofikiriwa wakati anajiunga na klabu hiyo baada ya kufukuzwa katika klabu El-Merrekh ya nchini Sudan.
Nabi alijiunga na Yanga sc Aprili mwaka jana na mpaka sasa anakaribia kufikisha mwaka mmoja klabuni hapo ambapo licha kutotwaa taji lolote la maana zaidi ya ngao ya jamii akiifunga Simba sc 1-0 bao la Fiston Mayele lakini mwanga umeanza kuonekana klabuni hapo ambapo timu hiyo sasa inacheza soka la kuvutia na kuwavutia mashabiki na viongozi wa klabu hiyo akiwemo tajiri Gharib Said Mohamed.
Mpaka sasa Nabi ameiongoza klabu ya Yanga sc katika mechi 21 za ligi kuu nchini na kombe la shirikisho ambapo katika mechi hizo ameshinda jumla ya mechi 15 na kufunga magoli 31 huku akisuluhu michezo 3 huku hakupoteza hata mchezo mmoja.
Licha na kukabiliwa na majeraha ya wachezaji muhimu kikosini kocha huyo ameibuka katika nyakati ngumu kwa kushinda michezo muhimu dhidi ya Mtibwa Sugar,Geita Sugar na mchezo dhidi ya Kmc kwa mabao 2-0 mabao ya kujifunga ya Andrew Vicent na bao la kichwa na Djuma Shabani yakitosha kabisa kupeleke ushindi jangwani.
Mtihani mkubwa kwa Nabi ni mchezo unaofata dhidi ya Azam Fc aprili 6 huku pia akitarajiwa kukutana na Simba sc Aprili 30 ambapo mpaka sasa Yanga sc ipo kileleni kwa alama 48.