Connect with us

Makala

Mayele Akabidhiwa Ng’ombe Dar

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Fiston Mayele amekabidhiwa ng’ombe wake aliyeahidiwa na shabiki wa klabu hiyo baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa sugar ambapo Yanga sc iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Baada ya mchezo kumalizika shabiki huyo alijitokeza na kuahidi kutoa zawadi hiyo kwa Mayele ambaye alifunga bao moja kati ya mabao mawili ya klabu yake ambapo hatimaye leo Ng’ombe huyo amekabidhiwa rasmi kwa Mayele jijini Dar es salaam katika makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani.

Pia shabiki huyo pamoja na kutoa zawadi ya Ng’ombe kwa Mayele pia alitoa zawadi ya mbuzi kwa ajili ya pole kwa bosi wa kampuni ya Gsm bwana Gharib Said Mohamed kutokana na kufiwa na baba yake mzazi mzee Said Mohamed wiki chache zilizopita.

Baada ya kukabidhiwa zawadi hiyoMayele amesema kuwa zawadi hiyo ni pongezi kubwa na inaongeza morali kwake pamoja na wachezaji kiujumla.

“Ni furaha kwetu kuona zawadi nimepata na ni kwa ajili ya kuongeza morali hivyo tutazidi kupambana zaidi kupata matokeo,” amesema Mayele.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala