Connect with us

Makala

Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Wafungiwa

Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi uliopo mkoani tabora umefungiwa kitumika katika michezo ya ligi kuu ya Nbc nchini pamoja na kombe la Shirikisho la Crdb kutokana na kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu nchini.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi kuu nchini imesema kuwa uwanja huo haukidhi matakwa ya Kanuni kama zilivyoanishwa katika masharti ya kanuni za leseni za klabu nchini.

Katika Taarifa hiyo bodi ya ligi kuu imeshauri klabu zote zinazotumia uwanja huo katika michezo ya nyumbani zitalazimika kutafuta uwanja mwingine mpaka uwanja huo utakapofanyiwa ukarabati na kufunguliwa.

Kutokana na Taarifa hiyo klabu ya  Tabora United sasa italazimika kutafuta uwanja mwingine katika michezo ya ligi kuu iliyosalia hapa nchini.

Taarifa hiyo imekua mwiba kwa mashabiki wa soka mkoani Tabora kutokana na kutemea timu ya Yanga sc kucheza mkoani humo katika mchezo wa marudiano dhidi ya Tabora United hasa baada ya kushinda 3-1 katika mchezo wa awali katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala