Connect with us

Makala

Mapro 12 sasa Ruksa

Bodi ya ligi kuu nchini (TPLB) imetangaza mabadiliko ya kanuni za usajili wa wachezaji wa kigeni ambapo klabu sasa zinaruhusiwa kusajili wachezaji 12 wa kigeni huku wakiruhisiwa kuwatumia wote katika mchezo mmoja tofauti na awali ambapo walikua wanaruhusiwa wachezaji 8 pekee.

Mabadiliko hayo yamekuja baada ya kikao na wadau wa ligi kuu wakiwemo viongozi wa klabu zote za ligi kuu nchini ambapo klabu zilikubali mapendekezo hayo.

Klabu za Simba sc,Yanga sc na Azam Fc ndio wafaidikaji wakubwa wa mabadiliko hayo kwa wana wachezaji wengi wa kigeni kiasi kuna kipindi kanuni ilikua inawabana katika uchaguzi wa kikosi na kufanya baadhi ya mastaa kukaa jukwaani licha ya kusajiliwa kwa pesa nyingi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala