Connect with us

Makala

Maki Awakalia Kooni Mastaa Simba sc

Kocha wa klabu ya Simba sc Zoran Maki amewakalia kooni baadhi ya mastaa wa klabu hiyo kutokana na kutoridhishwa na viwango vyao licha ya kuwa wamesajiliwa kwa pesa ndefu huku wakiwa hawajaitumikia klabu hiyo kwa kiasi kikubwa.

Maki ambaye alijiunga na Simba sc mwanzoni mwa msimu huu na kukuta baadhi ya mastaa tayari wamesajiliwa kikosini hapo imebainika kuwa haridhishwi na viwango vya mastaa kama Cletous Chama,Moses Phiri,Nassoro Kapama,Victor Akpan na Jonas Mkude hivyo kuhitaji baadhi yao waondolewe haraka.

Tayari uongozi wa klabu hiyo umewataarifu Victor Akpan na Nassoro Kapama watafute timu za kujiunga ama jumla au kwa mkopo huku nafasi hizo zikitarajiwa kujazwa na Mudathiri Yahaya na kiungo mwingine wa kigeni ambapo tayari kuna mazungumzo na Wanaijeria kuja kujaza nafasi hiyo.

Kwa upande wa Chama na Phiri uongozi wa klabu hiyo umemwambia kocha huyo kutafuta namna ya kuwatumia kwani usajili wao umegharimu pesa nyingi huku viwango vyao havipo chini bali ni mfumo wa kuwatumia tu.

Pia kocha Maki ameonyeshwa kutoridhishwa na Jonas Mkude hasa katika kutimiza majukumu ya ukabaji hivyo anajitahidi kumbadilishia majukumu kwenda kucheza kama namba nane akiwa na kazi ya kushambulia zaidi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala