Connect with us

Soka

Julio Atambulishwa Rasmi Singida Fg

Kocha Jamhuri Kihwelu ametambulishwa kama kocha mkuu wa klabu ya Singida Fountain Gate Fc akichukua nafasi ya kocha Thabo Senong ambaye alitimuliwa kufuatia matokeo mabaya ya timu hiyo katika siku za karibuni hasa tangu ligi irejee baada ya mapumziko ya kupisha michuano ya Afcon.

Julio atasaidiwa na kocha Ngawina Ngawina ambaye alisimama kama kocha mkuu wakati timu hiyo ikicheza na Simba sc katika mchezo ambao ilifungwa kwa mabao 3-1 licha ya timu hiyo kucheza vizuri kipindi cha pili.

Julio atakua na kazi ya kuhakikisha kikosi hicho kinafanya vizuri katika michezo takribani kumi iliyosalia ya ligi kuu nchini ambapo mpaka sasa kikosi hicho kipo nafasi ya 12 ya msimamo kikiwa na alama 21 katika michezo 20 ya ligi kuu ya Nbc.

Timu hiyo imekua na matokeo yasiyoridhisha baada ya kuwatoa mastaa wake takribani watano ambao wamejiunga na Ihefu Fc katika dirisha dogo la usajili huku pia ikitajwa kuwa imeshusha hata mishahara ya baadhi ya mastaa kutokana na ukata wa fedha.

Mastaa kama Marouf Tchakei,Abdalah Khomeiny,Joash Onyango,Duke Abuya,Morice Chukwu ni moja ya wachezaji waliokua na msaada klabuni hapo hivyo tangu waondoke na kujiunga na Ihefu Fc kikosi hicho kimeyumba.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka