Connect with us

Makala

Yanga Sc Yafungiwa Tena

Ikiwa tayari ina kesi ya kulipa fedha kwa ajili ya mshambuliaji Lazarus Kambole bado klabu ya Yanga sc imeandamwa na madeni ya kulipa fedha za kuvunja mikataba ya baadhi ya mastaa wa klabu hiyo na sasa inadaiwa na klabu ya Benchem United kulipa kiasi cha dola laki moja kwa ajili ya usajili wa Augustine Okrah.

Iko hivi mabosi wa Yanga sc walimsajili staa huyo kwa dau la dola laki moja na elfu ishirini huku wakilipa dola elfu ishirini pekee na kubaki na deni la dola laki moja ambazo wanapaswa kuzilipa na klabu hiyo tayari imekwenda Fifa kushtaki ikidai fedha hizo.

Inasemekana mabosi wa Yanga sc wanapambana ili kuachana na Okrah msimu huu kwa makubaliano ya pande mbili lakini ugumu unakuja kulipa gharama hizo za kimkataba kwa mchezaji huyo sambamba na kuilipa klabu yake kiasi hicho cha fedha.

Kutokana na hilo klabu hiyo moja kwa moja itaingia matatani kufungiwa kusajili kwa mara nyingine ambapo hivi sasa wana kesi ya usajili wa Kambole ambaye amesababisha klabu hiyo kufungiwa kusajili mpaka hapo itakapolipa deni hilo.

Hata hivyo taarifa kutoka Ghana zinasema kwa Yanga sc pia ijiandae na kesi ya Hafidh Nkonkoni ambaye naye ilimtema msimu huu wakati wa dirisha dogo kupisha usajili wa mastaa wengine baada ya kocha Miguel Gamondi kushindwa kumpa nafasi kikosini ambapo baada ya kutolewa kwa mkopo sasa staa huyo anajiandaa kukimbilia Fifa kushtaki akidai malipo ya fedha za usajili,Bonansi na mishahara.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala