Connect with us

Soka

Zidane hana mpango na Man Utd

Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane hana mpango wa kuwa kocha mkuu wa Manchester United kwasasa baada ya timu hiyo kuwania saini yake kumrithi Ole Gunnar Solskjaer aliyefukuzwa kazi.

Ole alifutwa kazi siku ya Jumapili baada ya matokeo mabovu ya kufungwa 4-0 na Watford katika mchezo wa mwisho wa ligi.

Zidane hana kazi kwasasa baada ya kuachana na Madrid baada ya kumalizika kwa msimu uliopita,na kocha huyo hataki kuchukua majukumu ya ukufunzi katikati mwa msimu.

Kikwazo kingine ni kocha huyo kutokuwa na uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiingereza,kitu ambacho anafanyia kzi sasa kwa kuchukua kozi ya lugha hiyo.Hata hivyo Zidane anatamani zaidi kufanya kazi PSG kuliko kwenda Uingereza.

Man Utd kwasasa inatafuta kocha wa muda atakayeiongoza timu hiyo hadi mwisho wa msimu,huku Michael Carrick akitekeleza majukumu ya kuinoa timu hiyo muda huu ipo sokoni kumtafuta mrithi wa Ole.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka