Connect with us

Soka

Yondani Awatega Vigogo Yanga sc

Viongozi wa Yanga wapo mtegoni kufuatia ripoti ya kocha Luc Eymael kumtaja Kelvin Yondani katika orodha ya mastaa ambao anaweza kuwatema ili kusajili vifaa vipya klabuni hapo.

Licha ya ripoti hiyo kuonyesha hivyo taarifa za ndani kutoka katika kamati ya usajili ya klabu hiyo zinadai baadhi ya wajumbe wameonyesha kutokubaliana na uamuzi huo kutokana na ukongwe wa staa huyo klabuni hapo.

Pia imetajwa kitendo cha kumuacha beki huyo ni kurudia makosa yaliyofanywa na klabu ya Azam fc ambayo iliachana na wakongwe na kuwauzia silaha wapinzani wao Simba sc ambao waliwasajili na kufanikiwa kuchukua ubingwa mara mbili mfululizo.

Tayari beki huyo ameshafahamu mpango huo wa kumtema na ameshaanza kuangalia malisho mengine huku Simba ikiwa kipaumbele chake.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka