Connect with us

Soka

Yanga yasaini mkataba kadi za wanachama

Klabu ya soka ya Yanga imeingia mkataba na makampuni ya Kilinet na N-Card kwaajili ya utengezaji wa kadi za wanachama wa klabu hiyo ikiwa ni sehemu ya hatua za awali kwenye mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Kadi hizo zitakuwa zikipatana kupitia matawi rasmi ya klabu hiyo nchi nzima,baada ya anayehitaji kufanya malipo kupitia njia ya benki au mitandao ya simu,zitakuwa zikiuzwa kwa gharama ya Tsh 29,000 tu kwa kadi moja.

Wiki chache zilizopita klabu hiyo iltangaza kutiwa saini kwa katiba mpya ya mfumo wa uendeshaji wa klabu pamoja na kusajiliwa rasmi na baraza la michezo nchini(BMT),kitu ambacho kimewezesha kuanza kwa zoezi la utoaji wa kadi za kisasa za kidijitali.

Kazi nyingine kubwa kwa kampuni ya Kilinet itakuwa ni kusimamia mchakato wa utekelezaji wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kidijitali ili kuhakikisha unakuwa rahisi na unafanikiwa kwa haraka zaidi kulingana na muda waliojiwekea uongozi mzima wa klabu hiyo yenye makazi yake Twiga na Jangwani Jijini Dar es salaaam.

Mwanachama anapaswa kuchukua kwanza fomu za uanachama kupitia matawi rasmi ya klabu hiyo nchi nzima yatakayomuwezesha kupata kadi hiyo kwa urahisi.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka